• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Waziri Bashungwa atoa maagizo mazito kwa maafisa elimu Mkoa na wathibiti ubora

Imewekwa tar.: January 14th, 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa  amewaagiza  Maafisa wa Elimu wa Mikoa na Wilaya,  nchini kuwasimamia Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu wa Masomo, kuzingatia kalenda ya utekelezaji wa mtaala, ili kuwa na ufundishaji na ujifunzaji wenye tija na mahiri.

Akizundua  kalenda  za utekelezaji  wa mitaala  na mafunzo  kwa Maafisa  Elimu  wa Mikoa na Wathibiti Wakuu wa  Ubora wa Shule Kanda leo Jijini Dodoma leo  Waziri Bashungwa amewaagiza Maafisa Elimu Mikoa, kutoa mafunzo ya matumizi ya Kalenda ya Utekelezaji, katika Halmashauri zenu zote, kabla au ifikapo tarehe 1 Februari, 2022.

Waziri Bashungwa ameitaka Mikoa na Halmashauri, kuwatambua wadau wote wa elimu, waliopo katika maeneo yao na kubaini miradi wanayoitekeleza, kwa kuitembelea na kufanya tathmini ili kuona kama miradi hiyo ina tija katika elimu na kuwaagiza  kuhakikisha taarifa za  utekelezaji wa miradi hiyo, iwasilishwe kwa Katibu Mkuu – OR TAMISEMI, kila baada ya miezi mitatu.

Kuhusu Michezo Waziri Bashungwa  ameiagiza  Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuhakikisha zinasimamia kikamilifu, ratiba ya shughuli za michezo, kwa Shule za Msingi na Sekondari na kuwasisitiza kuzingatia ratiba ya michezo shuleni na kutekelezwa kikamilifu kwa kuwa michezo hutoa fursa kubwa ya kujiburudisha na kujifunza nje ya darasa.

Amewataka  Viongozi wa Mikoa, Halmashauri, Kata, Vijiji na wamiliki wa Shule, kuhakikisha wanasimamia kikamilifu utekelezaji wa sera, sheria, miongozo na maelekezo yote ya Serikali, ili kuwe na ufundishaji na ujifunzaji wenye tija na kuwasisitiza kutumia kitabu cha majumuisho ya nyaraka na miongozo ya elimu toleo Namba 1 la Oktoba, 2021, kilichotolewa na OR-TAMISEMI kama rejea katika utekelezaji wa elimu msingi.

Waziri Bashungwa amewaagiza  viongozi wa Mikoa , Halmashauri na wakuu wa shule  kuhakikisha kutokuwepo na mwanafunzi yeyote  wa awali, darasa la kwanza  au kidato cha kwanza anatozwa michango kama sharti  la mwanafunzi  kuandikishwa na kila shule kuhakikisha inakuwa na mwalimu mmoja kwa ajili ya kuandikisha wanafunzi kipindi hiki  cha likizo.

“Ninawaagiza Viongozi wote wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa mwongozo wa utoaji wa Elimumsingi Bila Malipo, kwa kuwa Mheshimiwa Rais ameongeza fedha zinazotolewa kila mwezi, kwa ajili ya kugharimia elimu bila malipo, kutoka shilingi bilioni 23 kwa mwezi hadi kufikia bilioni 26 kwa mwezi na niwatake kuendelea kufafanua utekelezaji wa waraka huo kwa wazazi” amesisitiza Waziri Bashungwa

Waziri Bashungwa amewaagiza Maafisa Elimu wa Kata kwa kushirikiana na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji, kubainisha watoto wote wanaotakiwa kuandikishwa shule wakiwemo watoto wenye mahitaji maalum  na kuwasisitiza wazazi kuhusu umuhimu  wa kuwaandikisha watoto mashuleni.

Aidha,  amewaagiza kuhakikisha wanabandika  namba za simu za Kituo cha Huduma kwa Mteja katika kila Ofisi iliyo chini ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI, na vituo vyote vya kutolea huduma ikiwemo Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali, Shule, na Ofisi za Watendaji katika ngazi zote.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - AJIRA YA MKATABA LISHE July 03, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • SERIKALI KUENDELEA KUSOGEZA HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII KWA WANANCHI.

    July 01, 2025
  • Maafisa lishe watakiwa kumaliza udumavu, ukondefu kwa Watoto, vitambi na vilibatumbo kwa watu wazima

    July 01, 2025
  • WAZIRI MCHENGERWA AWAFUNDA MA RC WAPYA

    June 28, 2025
  • SERIKALI YAIPONGEZA TARURA KWA KAZI NZURI WANAZOFANYA MHE: MCHENGERWA AWASIHI KUTOKATISHWA TAMAA

    June 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.