• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

MIRADI YA TACTIC IMELETA MAPINDUZI YA KIUCHUMI MAJIMBONI KWETU- WABUNGE

Imewekwa tar.: June 26th, 2025

Dodoma

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameeleza mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii yaliyojitokeza ikiwemo fursa za kiuchumi inayotokana na kuboreshwa kwa mazingira ya ufanyaji wa biashara katika majimbo yao tangu kuanza kutekelezwa kwa mradi wa Uboreshaji wa miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) kwa awamu ya kwanza na ya pili ya mradi huo.

Wameyasema hayo jana Juni 25, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma wakati wa utiaji saini mikataba kwa Miji 11 ya Tanzania Bara, ambayo ni Morogoro na Songea kwa awamu ya kwanza pamoja na Miji ya Tanga, Korogwe, Babati, Shinyanga, Bukoba, Bariadi, Lindi, Iringa na Njombe.

Wabunge wanufaika wa miradi hiyo wameeleza kuwa TACTIC imesaidia katika kuboresha usimamizi na ukuaji wa miji sambamba na kuboresha utoaji wa huduma zinazotolewa na halmashauri zao kwa wananchi.

Mbunge wa Tanga mjini, Mhe. Ummy Mwalimu, miongoni mwa Viongozi wanufaika wa ujenzi wa mifereji ya maji, taa za barabarani na barabara za lami, amebainisha pia kuwa ujenzi wa Soko la Makorora na Soko la Samaki la Deep Sea mjini Tanga ilikuwa ni ndoto na kilio cha muda mrefu na kubainisha kuwa kukamilika kwake kutabadilisha hadhi na muonekano wa mji wa Tanga na kuongeza kipato kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wa mji huo kutokana na mazingira yao ya biashara kuwa ya kisasa na yenye kuvutia. 

Kwa upande wake, Mbunge wa Iringa mjini, Mhe. Jesca Msambatavangu amebainisha kuwa kujengwa kwa soko la Kihesa kwenye mradi wa TACTIC awamu ya pili kutaondoa adha ya wajasiriamali kufukuzwa na mgambo wa mji kutokana na kufanya biashara maeneo yasiyokuwa rasmi katikati ya mji pamoja na kukuza mzunguko wa fedha na uchumi wa Iringa mjini.

Aidha, mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhe. Msambatavangu pia ameeleza kuwa ujenzi wa barabara ya Mkimbizi – Bima, Mtwivila, Viziwi na barababara ya Bontank kutainufaisha zaidi Iringa kiuchumi na Kiutalii, na hivyo kupendezesha mandhari ya mji wa Iringa pamoja na kuimarisha shughuli za kiutalii katika mji huo ulio kitovu cha utalii kwa kanda ya Kusini.

Kwa upande wake, Mbunge wa Bukoba mjini, Steven Byabato na Mhe. Patrobas Katambi mbunge wa Shinyanga mjini, nao wameshukuru kwa ujio wa miradi ya TACTIC katika miji yao wakimshukuru Rais  Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuongoza mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kustawisha jamii kupitia miradi ya TACTIC, kwa lengo la kuboresha miundombinu ya miji 45 ya Tanzania pamoja na kujenga uwezo wa halmashauri ili ziweze kujiimarisha na kutoa huduma zenye ubora kwa wananchi wanaowahudumia.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - AJIRA YA MKATABA LISHE July 03, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • SERIKALI KUENDELEA KUSOGEZA HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII KWA WANANCHI.

    July 01, 2025
  • Maafisa lishe watakiwa kumaliza udumavu, ukondefu kwa Watoto, vitambi na vilibatumbo kwa watu wazima

    July 01, 2025
  • WAZIRI MCHENGERWA AWAFUNDA MA RC WAPYA

    June 28, 2025
  • SERIKALI YAIPONGEZA TARURA KWA KAZI NZURI WANAZOFANYA MHE: MCHENGERWA AWASIHI KUTOKATISHWA TAMAA

    June 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.